Masomo ya Misa Mei 12

[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 12/05/2024

2024 MEI 12 : DOMINIKA YA 7 YA PASAKA

KUPAA BWANA
Rangi: Nyeupe

Zaburi: Tazama sala ya siku

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/ascension_2018_hd-678×380-1.jpg” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”ascension_2018_hd-678×380″ hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″ animation_style=”bounce”][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Somo 1. Mdo 1:1-11

Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi,  baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohane alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/50c12e479bb5110e2d2f67ed2be69dae.jpg” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”50c12e479bb5110e2d2f67ed2be69dae” animation_style=”bounce” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Wimbo wa Katikati. Zab 47: 2-3, 6-9

1. Enyi watu wote, pigeni makofi,
Mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe,
Kwa kuwa Bwana aliye juu, mwenye kuogofya,
Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.

(K) “Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti ya baragumu.”

2. Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,
Bwana kwa sauti ya baragumu.
Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;
Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni. (K)

3. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,
Imbeni kwa akili.
Mungu awamiliki mataifa,
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. (K)

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Somo 2. Efe 1:17-23

Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Injili. Mk 16:15-20

Yesu alionekana na wale kumi na mmoja, akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/1297552532614_ORIGINAL.webp” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”1297552532614_ORIGINAL” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″ animation_style=”bounce”][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

TAFAKARI

AMEPAA NA KUTUACHIA SISI UWANJA WA KUMTANGAZA
Siku arobaini baada ya Ufufuko wa Kristo Kanisa huadhimisha Sherehe ya kupaa Bwana mbinguni. Katika sala ya mwanzo ya sherehe ya leo tumesema: “huko alikotutangulia yeye kichwa chetu, ndiko tunakoamini kufika sisi tulio mwili wake.” Tunaadhimisha tukio la furaha sana katika historia ya ubinadamu wetu kwani mbingu na dunia vinaungana tena. Yeye aliyeutwaa ubinadamu wetu anakuwa mwakilishi wetu huko juu mbinguni. Ubinadamu wetu uliokombolewa, ulio katika hali ya utukufu wa ufufuko sasa unakaa pamoja na Mungu huko juu mbinguni.
Somo la kwanza linatupatia mambo mawili: kwanza linatupatia hakika ya kwamba huyu aliyepaa mbinguni ni Kristo Mfufuka. Anapaa mbinguni baada ya ufufuko wake na baada ya kuwahakikishia wafuasi wake kuwa ni Yeye kweli amefufuka: “aliwadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyohusu ufalme wa Mungu.” Dokezo hili ni muhimu katika imani yetu kwani tunaitafakari hadhi yake huyu anayepaa mbinguni. Yupo katika mwili wa utukufu na anapaa kwenda kuungana na Baba aliye mtukufu. Ni dokezo kwetu kuwa ni katika hali hiyo ya utukufu ambayo tunarithishwa kwa njia ya Kristo katika Roho Mtakatifu ndipo nasi tunaungana na Mungu.
Ufufuko wa Kristo unapyaisha tena ubinadamu wetu ambao ulichakazwa na dhambi. Mwili wake wa utukufu hauchangamani tena na dhambi bali unakwenda kuungana na Mungu mtukufu. Hadhi hii inapasika kuhisiwa na binadamu wote na kusema kwa shangwe kubwa kama Papa Leo mkuu: “Ewe Mwanadamu, kitambue cheo chako.” Cheo chetu ambacho tulikuwa nacho tangu wakati wa uumbaji ni kuwa pamoja na Mungu. Dhambi ndiyo ilimfukuzisha mwanadamu kutoka bustani ya Edeni mahali ambapo Bwana Mungu alimwandalia mwanadamu na daima alimtembelea.  Baada ya dhambi ya kwanza Mungu “alimtoa mwanadamu katika bustani ya Edeni, alime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima” (Mwa 3:23 – 24). Kwa ufufuko na kwa kupaa kwake mbinguni Kristo anamrudisha tena mwanadamu katika kutaniko hili la Mungu.
Katika somo la Injili tunatumwa kwenda kuitangaza habari njema. Kristo mfufuka kabla ya kupaa mbinguni anawatuma mitume wake, ambao ni jamii ya kwanza ya wanadamu kushirikishwa hali yake ya kimungu, kuisambaza habari njema yaani wokovu wa mwanadamu kwa watu wote. Hili ni dokezo muhimu kwamba Yeye hakuja kwa ajili ya kuwapeleka wachache (kikundi kidogo alichokuwa nacho wakati wa maisha yake hapa duniani) mbinguni bali kwa ajili ya wanadamu wote kinachosalia kwa wanaotangaziwa habari hii njema ni kuipokea ili waokoke au kuikataa ili kupata hukumu.
Kristo anapopaa mbinguni anakwenda kututayarishia makao. Yeye mwenyewe aliahidi akisema kwamba “naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwanu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo” (Yn 14: 2-3). Kabla ya kupaa kwake alituthibitishia kuwa anakokwenda ni kwa Baba yake na Baba yetu, kwa Mungu wake na Mungu wetu (rej. Yn 20:17). Hii ni ahadi ya matumaini na sababu ya kupata nguvu kwenda kuitangaza Injili ya Kristo. Ni ahadi inayotupatia nguvu kwani tunaona moja kwa moja tunaitangaza habari inayotuhusu sisi wenyewe kwani tunayemtangaza ameungana nasi, ni Kristo ndugu yetu na mwishoni tutamkuta anatusubiri mbinguni kwa Baba yake na Baba yetu. Hivyo utume wetu wakristo ni kwenda kushuhudia na kuifunua hadhi hiyo kwa watu wote.
Ushuhuda wa upya wa maisha hujidhihirisha kwa namna nyingi lakini Kristo aliweka upendo kuwa njia mahsusi ya utambulisho wetu: “Watu watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi” (Yn 13:35). Utangazaji wetu wa habari njema utapata nguvu zaidi katika matendo yetu mema yanaoufunua upendo wa Mungu kwa wengine. Katika nyakati zetu hizi tumekuwa na mabingwa walioonesha kwamba kweli sasa ubinadamu umeungana na umungu. Kati yao ni Mama Theresa wa Calcutta ambaye mkutano wake wa ndani na Kristo umemfanya kuwa kioo cha utume wa upendo kwa watu wote hasa maskini na wanaoteseka na alama ya ukristo wetu kwa watu wote. Ulimwengu umeitambua tunu iliyopo ndani mwake; ulimwengu umeonja kwamba kweli umungu na ubinadamu umekutana kwani wote waliuonja upendo wa Mungu kupitia nafsi ya Mama huyu Mtakatifu.
Tunapoalikwa leo hii kuwa mashuhuda wa upya huo tunapokea changamoto kubwa. Tunashuhudia leo hii watoto wengi wanateseka na kukosa haki zao za msingi, wanawake wengi wananyimwa haki zao, wanyonge wengi wanazidi kudidimizwa kwa vitendo vya rushwa. Katika neno moja ni kwamba, tunashuhudia ubinadamu uliojeruhiwa. Katika hali hii hamu ya upendo wa Mungu inatawala mioyo yao. Mwanadamu katika mazingira haya ana kiu ya kumwona Mungu. Furaha ya sherehe ya leo itapata maana pale tutakapowashirikisha wenzetu katika hali hiyo ya mahangaiko tone la upendo wa Mungu. Sisi tunafurahi na tunapata nguvu sababu tumehakikishiwa kuwa ubinadamu umeungana na umungu lakini furaha hii si yetu binafsi, ni zawadi ambayo inatuita kutoka nje na kuwashirikisha wengine.
Mausia ya Mtakatifu Paulo katika somo la pili yawe dira kwetu. Tuiombe roho ya hekima na kuujua ukuu tuliofanyiziwa. Tujitoe bila kujibakisha katika utume wetu ili kumshuhudia Yeye aliyepaa mbinguni kututayarishia makao. Hilo litakuwa ni tendo la shukrani kwetu kwani huduma yetu hiyo itawafikia wote na hivyo malengo ya utumishi wake, yaani wokovu kwa watu wote yatatimia. Mwishoni kama tulivyoomba katika sala ya mwanzo tutafika huko alikotutangulia Yeye aliye kichwa chetu.

SALA: Ee Bwana Yesu utujalie hamu ya kwenda mbinguni.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these