Description
Katika Injili ya Mathayo (13:5) anatajwa kama “fundi”, (kwa Kigiriki). Lakini inasema pia (sawa na Injili ya Luka) kuwa alitoka katika ukoo wa mfalme Daudi.
Injili na imani ya Kikristo zinasisitiza kuwa baba halisi wa Yesu alikuwa Mungu mwenyewe: Maria alimchukua mimba kwa muujiza uliosababishwa na Roho Mtakatifu.
Ndoto ya Mt. Yosefu, mchoro wa Josè Luzan
Yosefu, kisha kujulishwa juu ya mimba hiyo, alikubali kumchukua mchumba wake nyumbani na kumtambua mwanae kuwa ni wa kwake ingawa hakuwahi kujamiana naye. Hivyo alitunza heshima ya mama na mtoto na kuwahakikishia ulinzi katika jamii inayojali zaidi wanaume.
Miezi baadaye familia yake ilikwenda Bethlehemu kwa ajili ya sensa, na ndipo Yesu alipozaliwa pangoni na kulazwa horini.