JUMATATU: JUMA IV LA MWAKARANGI: KIJANIKUMBUKUMBU YA HIYARIZABURI: JUMA IV Mt. BlasiUtume: Alikuwa Askofu wa Sebaste huko Armenia (Uturuki). Blasi alikuwa imara katika imani na alikufa kwa kukatwa kichwa. Alikufa
DOMINIKA YA 4 YA MWAKA
Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa amani, kama ulivyosema; kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, uliouweka tayari machoni pa watu wote; nuru ya kuwa mwangaza wa mataifa, na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Masomo ya Misa Januari 31
Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.
Masomo ya Misa Januari 30
Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa. Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Masomo ya Misa Januari 29
Na hawa ndio, waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikialo lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.
Masomo ya Misa Januari 28
Tazama, mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
Januari 27
Awezaje Shetani kumtoa Shetani? Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama; na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
Dominika ya 3
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.
Januari 25
“Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.”
Januari 24
Mt. Fransisko alizaliwa katika mji wa Sale (Ufaransa). Wazazi wake walimlea kitajiri kama ilivyokuwa hali yao. Lakini Mungu alikuwa akimvuta Fransisko rohoni, hata aliacha dunia akaingia upadre. Alianzisha shirika la masista wa Maonano. Neno lake kuu lilikuwa: “Kufanya kitu kwa wema na upole”.