Masomo ya Misa Septemba 30

[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 30/09/2024

2024 SEPTEMBA 30: JUMATATU-JUMA LA 26 LA MWAKA

Mt. Hieronimo, Padre na Mwalimu wa Kanisa
Rangi: Nyeupe

Zaburi: Juma II

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/09/maxresdefault-1-1.jpg” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”maxresdefault (1)” animation_style=”bounce” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

SOMO 1. Ayu 1:6-22

Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza, Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, “Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.” Kisha Bwana akamwuliza Shetani, “Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.” Ndipo shetani akamjibu Bwana, na kusema, “Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.” Bwana akamwambia shetani, “Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe.” Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana. Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng’ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.” Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, “Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.” Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, “Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watushi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.  Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, “wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.”  Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka na nchi, na kusujudia; akasema, “Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko nili uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la bwana na libarikiwe.” Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

WIMBO WA KATIKATI. Zab 17:1-3, 6-7

1. Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio change,
Utege sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiyotoka katika midomo ya hila.

(K) Utege sikio lako ulisikie neno langu.

2. Hukumu yangu na itoke kwako,
Macho yako na yatazame mambo ya adili.
Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,
Umenihakikisha usione neno. (K)

3. Ee Mungu nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu;
Dhihirisha fadhili zako za ajabu,
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia. (K)         

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

INJILI. Lk. 9:46-50

Wanafunzi walianza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao. Naye Yesu alipotambua mawazo ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo akamweka karibu naye, akawaambia, “Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.” Yohane akajibu akamwambia; “Bwana mkubwa, tuliona mtu anatoa pepo kwa jina lako; tukamkataza, kwa sababu hafuatani na sisi.” Yesu akamwambia, “Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.”
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

TAFAKARI

TUMWAMINI MUNGU KATIKA KILA JAMBO: Kitabu cha Ayubu ni moja ya vitabu katika Agano Kale kilicho andikwa vizuri sana. Kinamzungumzia Ayubu mtu wa Mungu ambaye alitumia muda wa maisha yake hapa duniani akitenda mema. Alikuwa ni mtakatifu wa wakati wake. Siku moja anaanza kupokea mfululizo wa matukio yaliyo msononesha, ilikuwa ni hasara kubwa. Ayubu hakuelewa ni kwa nini anafikwa na majanga yaliyompata kwani amekuwa muda wote mwaminifu kwa Mungu. Alikuwa na mahangaiko makubwa, anatafufa majibu kwa rafiki zake na kwa Mungu, lakini hapati majibu ya kuridhisha. Kupitia haya matatizo anaendelea kumwamini Mungu. Imani ya Ayubu kwa Mungu ni sawa na imani ya mtoto kwa anayemwongoza. Watoto ni wanyoofu, watii, wakarimu, wanyenyekevu nk. Kwa kumweka mtoto katikati ya wanafunzi wake, Yesu anabadili mtazamo wao wa kufikiri juu ya ukubwa na kuwa ni ule wa aliye tayari kuwapokea wengine na kuwakusanya kwa unyofu na upendo, na sio mamlaka, madaraka na kutumikiwa.  

SALA: Ee Bwana neema yako itufundishe kuwa viongozi kwa tukiwatumikia wanajamii kwa upendo na unyenyekevu.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

You may also like these