Masomo ya Misa Novemba 7

[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 07/11/2024

2024 NOVEMBA 7: ALHAMISI: JUMA LA 30 LA MWAKA

Mt. Wilibrodi, Askofu
Rangi: Kijana

Zaburi: Juma III

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

SOMO 1. Flp 3:3-8

Sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu. 
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

WIMBO WA KATIKATI. Zab 105: 2-7

1. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

(K) Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

2. Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. (K)

3. Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake,
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye Bwana, ndiye Mungu wetu,
dunianai mwote mna hukumu zake. (K)

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

INJILI. Lk 15:1-10

Watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia Yesu wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. Akawaambia mfano huo, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmoja wapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. Au kuna mwanamke gani mwenye shillingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shillingi ile iliyonipotea. Nawaambia, vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.  
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

TAFAKARI

KUSHIRIKI HATIA: Katika kuchagua marafiki, kunahitajika busara ya hali ya juu. Wanamichezo wanashauriwa wasijihusishe na wanaocheza kamari. Kijana anayetembea na wale wanaouza au kutumia madawa ya kulevya, anakua katika hatari ya kuwa mmoja wao katika kuuza na kutumia madawa ya kulevya. Katika miji mikubwa wazazi na walezi wanawapiga marufuku vijana wao wasikae katika makundi ya wahuni mitaani. Lakini kwa Yesu haikuwa hivyo. Alitumia muda wake pamoja na wadhambi, ilikuwa ni sehemu ya utume wake kueneza Habari Njema kwa watu wote. Kanisa linapaswa kuwa kama kijito jangwani kwa ajili ya wadhambi na watu wengine walio waovu. Ni jambo rahisi kumwelewa Mungu anapowasamehe wadhambi wanaokimbilia huruma yake. Mungu ambaye anawatafuta wadhambi na kwa furaha kuwasamehe, lazima awe na upendo wa pekee. Upendo huu ndio uliomsukuma Yesu kuwatafuta wale waliopotea na kuwakomboa. Huo ndio upendo alionao Mungu na kama unaonja hilo, usikate tamaa. Mungu anakutafuta, nawe uwatafute waliopotea. 

SALA: Ee Mungu unijalie moyo wa kuwapenda walio waovu na kujitahidi kuwatafuta na kuwarudisha kwako.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

You may also like these