[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 01/11/2024
2024 NOVEMBA 1: IJUMAA: JUMA LA 30 LA MWAKA
WATAKATIFU WOTE
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Tazama sala ya siku
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
SOMO 1. Ufu 7:2-4, 9-14
Mimi Yohane, niliona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na mwana-kondoo. Na malaika wote walikuwa wakisimama upande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, na wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, wakisema, Amina; baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina. Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Nao wametoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
WIMBO WA KATIKATI. Zab 24:1-6
1. Nchi na vyote viijazavyo nui mali ya Bwana, (K) Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana. 2. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? 3. Atapokea baraka kwa Bwana, |
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
SOMO 2. 1 Yoh 3:1-3
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo mtakatifu. |
[/et_pb_text][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
INJILI. Mt 5:1-12
Yesu alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
TAFAKARI
KUTENDA KIPEKEE: Wale wanaotaka kuishi kwa ajili ya Mungu, wanapaswa kuwa tayari kusema na kutenda katika namna ile inayoonekana ni ya kipekee kwa ulimwengu. Wakristo wnapaswa kuwa tayari kutoa pale wangine wanapochukua, kupenda pale wengine wanapochukia, kusaidia pale wengine wanaposhindwa kusaidia. Kwa kuweka kando ubinafsi kusudi waweze kuwasaidia wengine. Siku moja tutapokea kila kitu ambacho Mungu alituwekea tayari. Tunapotafuta furaha na matumaini vilivyo kiwango kikubwa kabisa cha furaha, ni lazima tumfuate Yesu hata kama itatugharimu kiasi gani. Tunapaswa kuwa na njaa sio ya upendo kwa mtu fulani au njaa ya chakula bali tunapaswa kuwa na njaa na kiu ya haki. Jambo hilo hatulisikii mara kwa mara. Hatupaswi kuwa na njaa ya kupata haki yetu wenyewe tu bali haki yaw engine pia. Hatupaswi kujisifia maadili yetu. Wakristo wanaokua katika kumfuata Bwana wanahitaji kile ambacho Bwana anakitaka. Pale uovu unapotokea wanakuwa na njaa ya kuumaliza uovu huo. Wanataka Mungu awe mshindi dhidi ya uovu. Utakatifu ni ushindi dhidi ya maovu. SALA: Ee Mungu utufanye tuwe watu wa haki na amani. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]