Masomo ya Misa Oktoba 30

[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 30/10/2024

2024 OKTOBA 30: JUMATANO: JUMA LA 30 LA MWAKA

Mt. Klaudius
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma II

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

SOMO 1. Efe 6:1-9

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana, kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

WIMBO WA KATIKATI. Zab 145: 10-14

1. Ee Bwana kazi zako zote zitakushukuru,
Wacha Mungu wako watakuhimidi,
Tutaunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.

(K) Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru.

2. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)

3. Bwana huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini. (K)  

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

INJILI. Lk 13:22-30

Yesu alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. Mtu mmoja akamwuliza, Je!  Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia wasiweze. Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango mkisema, Ee Bwana tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu. Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.2″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]

TAFAKARI

UTAFUTE UKOMBOZI: Watu wengi wanashituka na kupokea katika mtazamo hasi wazo kuhusu mlango mwembamba au tunaposema kwamba Yesu ndio njia pekee. Na wanapokea katika mtindo huo kwa sababu wanataka mlango ambao wameuchagua ndio uwe sahihi na sio ule wa Mungu. Alichokuwa anamaanisha Yesu sio kuwatupa watu wengine nje, au kufanya watu wapate ugumu katika kuingia au kuuona, hapana. Yesu alitaka kusisitiza kwamba mlango mwembamba upo wazi na ni Mungu anayefungua mlango na sio wanadamu. Mungu ndiye anayefanya ukombozi upatikane. Yesu anataka kutufundisha kwamba, hatujitengenezei ukombozi wetu wenyewe. Wote tunapaswa kuja kwa Mungu na kufuata masharti ya kuja kwake na sio Mungu kufuata kile tunachotaka sisi. Ni vigumu sana kufuata masharti ya mtu mwingine na ndiyo ugumu tunaoupata katika kumfuata Mungu. Hivyo tunakumbushwa kwamba tusiruhusu matakwa yetu yatutenge na Mungu.

SALA: Ee Bwana utujalie kuyatimiza mapenzi yako kila siku ya maisha yetu.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

You may also like these