Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 28/10/2024
2024 OKTOBA 28: JUMATATU: JUMA LA 30 LA MWAKA
WAT. SIMONI NA YUDA, MITUME
Rangi: Nyekundu
Zaburi: Juma II
SOMO 1. Efe 2:19-22
Tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 19:1-4
1. Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, (K) Sauti yao imeenea duniani mwote. 2. Hakuna lugha wala maneno, |
INJILI. Lk 6:12-16
Yesu aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume; Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, naYakobo na Yohane, na Filipo na Bartolomayo, na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote, na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti. |
TAFAKARI
SALI KWANZA: Yesu hakuwahi kuandika kitabu. Hakuwahi kuwa na mikutano ya kukuza kanisa au vikao vya uamsho. Hakuacha chati kwa ajili ya sisi kuifuata. Njia yake ya pekee kabisa ya kuanzisha kanisa lake ilikuwa ni watu wale aliowaita wamfuate. Watu hawa ndio walioacha historia ya kanisa lake. Yesu hakuwa na mpango mwingine zaidi ya huo na ndio sababu alitumia muda wake katika kusali kabla ya kuwachagua. Kuna tofauti kubwa sana jinsi kanisa linavyoendeshwa siku hizi. Kwanza tunafanya uamuzi kisha tunamwomba Mungu abariki maamuzi hayo. Tunategemeaje basi kwamba maamuzi hayo yawe na mafanikio? Tutegemee ufanisi katika kazi na afya ya kanisa, kama waamini tutafuata mtindo wa Yesu wa kusali kwanza na kisha kutenda. “Yesu aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.” Je! Unayo maamuzi makubwa katika maisha yako? Yaweke maamuzi hayo mbele za Mungu katika kwa sala. SALA: Bwana Yesu utukumbushe kusali kabla ya kufanya jambo lolote ili kazi zetu zipate kibali kwako. |