Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 14/10/2024
2024 OKTOBA 14: JUMATATU-JUMA LA 28 LA MWAKA
Mt. Kalisti I, Papa na Shahidi
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma IV
SOMO 1. Gal 4:22-24, 26-27, 31; 5:1
Imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana. Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 113: 1-7
1. Aleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, (K) Jina la Bwana lihimidiwe milele. 2. Toka maawio ya jua hata machweo yake 3. Ni nani aliye mfano wa Bwana, |
INJILI. Lk 11:29-32
Makutano walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, “Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona. |
TAFAKARI.
WALITAFUTA NA WAKAONA: Watu wa Ninawi pamoja na Malkia wa Kusini walimgeukia Mungu kwa viashiria vichache, kuliko vile ambavyo Yesu alikuwa akiwaonesha wasikilizaji wake. Miujiza pamoja na matendo makuu ambayo tunayaona kwa macho yetu na taarifa za kufufuka kwa Yesu kutoka katika wafu tumezisikia, tunaona nguvu za Roho Mtakatifu iliyoanzia siku ya Pentekoste ikifanya kazi hata sasa, tunaweza kusoma Biblia kwa urahisi kabisa tofauti na wale waliokuwa wakipata habari kwa masimulizi ya mdomo. Lakini pia tumeweza kujifunza kwa miaka elfu mbili mambo aliyofanya Yesu kupitia Kanisa lake. Pamoja na fursa na uelewa huu wote na mang’amuzi tuliyonayo sasa, tunapaswa kumpokea na kumwamini Yesu kwa moyo wote kwa sababu ya yale tuliyoyaona na kuyasikia. Kwa bahati mbaya haturidhiki tunataka kuona zaidi na zaidi. Yesu anasimama mwenyewe kama ishara kwa vizazi vvyote na mtu mwenye mamlaka. Mpatie Yesu nafasi. Msikilize na itikia wito wake. SALA: Ee Bwana Yesu utujalie tuweze kusadiki pasipo kungojea ishara. |