Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 24/09/2024
2024 SEPTEMBA 24: JUMANNE-JUMA LA 25 LA MWAKA
Mt. Rupert wa Saizberg
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma I
SOMO 1. Mit 21:1-6, 10-13
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; kama mfereji wa maji huugeuza po pote apendapo. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; bali Bwana huipima mioyo. Kutenda haki na hukumu humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka. Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, hata ukulima wa waovu, ni dhambi. Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti. Nafsi ya mtu mbaya hutamani maovu; jirani yake hapati fadhili machoni pake. Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima; na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa. Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya; jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia. Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 119: 1, 27, 30, 34-35,44
1. Heri wali kamili njia zao, (K) “Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Ee Bwana.” 2. Nimeichagua njia ya uaminifu, 3. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, |
INJILI. Lk 8:19-21
Walimwendea Yesu mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikao neno la Mungu na kulifanya. |
TAFAKARI
UKIPUUZA MASKINI NAWE UTAPUUZWA: Kristo anaendelea kuonesha kuwajali watu wote kwani anatuambia mama yake na ndugu zake ni wale walisikiao neno la Mungu na kulitenda. Kwa utume wake wa hapa dunia aliwapenda na kuwasaidia maskini. Somo la kwanza linatuhimiza kutenda haki na kuwajali wengine. Raisi wa zamani wa chuo cha Harverford aliyejulikana kama John Coleman alitaka kufahamu wale wasiokuwa na makazi katika jiji la ‘New York’ wanavyojisikia. Akaamua kukaa barabarani kwa siku kumi bila fedha wala malazi. Shajara ya hizo siku kumi ilichapishwa kwenye gazeti la “New Yorker.” Mwanzo mmoja ulisomeka “natembea taratibu zaidi, sioni tena umuhimu wa kukimbizana na taa za kuongozea magari barabarani, nilizoea kuangalia ninakovaa saa, lakini saa haipo tena na hata kama ingekuwapo haina maana tena. Kipima joto kimekuwa cha muhimu sana kwangu. Akirudi kwenye geti alilolizoea anamkuta mlinzi yupo mahali pake.” Siku hizo kumi zilimfanya Coleman kuwa na mtazamo tofauti. Aliwapenda na kuwahudumia zaidi maskini kuliko awali. SALA: Ee Bwana utuwezeshe kuwasikiliza kwa upendo watu tunaokutana nao, kuwaelewa na kuwasaidia kadiri ya uwezo wetu. |