[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 15/08/2024
2024 AGOSTI 15: ALHAMISI-JUMA LA 19 LA MWAKA
KUPALIZWA MBINGUNI BIKIRA MARIA
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Tazama Sala ya Siku
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/08/assumption-1617-660×350-1471236326-1.webp” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”assumption-1617-660×350-1471236326″ animation_style=”bounce” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Somo 1. Ufu 11:19, 12:1-6, 10
Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana. Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, “Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.” |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Wimbo wa Katikati. Zab 45:9-11, 15
1. Binti za wafalme wamo (K) Mkono wako wa kuume amesimama malkia, amevaa dhahabu ya Ofiri. 2. Naye mfalme atautamani uzuri wako, |
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Somo 2. 1 Kor 15:20-27
Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Injili. Lk 1:39-56
Mariamu aliondoka, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.” Mariamu akasema, “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele. Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, Kisha akarudi kwenda nyumbani kwake. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
TAFAKARI
UTII NI FADHILA YA WATAKATIFU: Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria. Sherehe hii ilitangazwa na Papa Pio (Pius) XII tarehe 1.11.1950 kwa hati inayoitwa Munificentissimus Deus yaani “Mungu Mkarimu.” Kwa tangazo hili, Papa Pio XII alitamka kwamba baada ya kifo chake, Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho. MISALE YA WAUMINI chapa ya sita (1991, uk. 871) inaandika: “Maria ameingia utukufu wa mbinguni, ameshirikishwa utukufu wa Mwanawe.” Maria amepalizwa mbinguni kwa sababu tokea mwanzo alitimiza matakwa ya Mungu kwa utii wote, akawa mfuasi namba moja wa Mungu. Maria ni mama yetu. Kwa maisha yake alituonyesha jinsi ya kumfuata Kristo, tupate kufika mbinguni. Sherehe hii ni ishara kwamba tunayo maisha yaliyotukuka ndani yetu. Tumezaliwa ili hatimaye baada ya maisha haya hapa duniani tushirikishwe taji la utukufu wa milele. Sherehe hii ni zawadi kwa kila mmoja wetu kwa sababu inatupa matumaini kwamba imani yetu si bure. Tumeumbwa ili kuishi milele. SALA: Ee Mama Bikira Maria Mpalizwa mbinguni utuombee ili nasi tuweze kufika mbinguni. |
[/et_pb_text][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/08/assumption-of-the-blessed-virgin-mary.jpg” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″ title_text=”assumption-of-the-blessed-virgin-mary” animation_style=”bounce”][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]