Masomo ya Misa Agost 13

[et_pb_section fb_built=”1″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_row column_structure=”2_5,3_5″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”2_5″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 13/08/2024

2024 AGOSTI 13: JUMANNE-JUMA LA 19 LA MWAKA

Mt. Ponsian, Papa na Hipoliti, Padre na Mashahidi
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma III

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column type=”3_5″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/08/big-Mt-18-1-5.10.12-14-tre-nho.jpg” title_text=”big-Mt-18-1-5.10.12-14-tre-nho” _builder_version=”4.27.0″ _module_preset=”default” hover_enabled=”0″ global_colors_info=”{}” sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”4_4″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Somo 1. Eze 2:8-3:4

Ezekieli aliisikia sauti, ikamwambia: mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho. Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake. Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!  Akaniambia, mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Akaniambia, “Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali. Akaniambia, mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli,” ukawaambie maneno yangu. 

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row column_structure=”1_2,1_2″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Wimbo wa Katikati. ” Zab 119:14, 24, 72, 103, 111, 131″

1. Nitalitangaza jina Bwana;
Mpeni ukuu Mungu wetu.
Yeye mwamba, kazi yake ni kamilifu;
Maana, njia zake zote ni haki.
Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,
Yeye ndiye mwenye haki na adili.

(K) Mausia yako matamu sana kwangu.

2. Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi;
Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;
Wazee wako, nao watakuambia. (K)

3. Yeye Aliye juu alipowapa mataifa urithi wao,
Alipowabagua wanadamu,
Aliweka mipaka ya watu
Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake,
Yakobo ni kura ya urithi wake. (K)

4. Bwana peke yake alimwongoza,
Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye. (K)

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Injili. Mt 18:1-5, 10, 12, 14

Wanafunzi walimwendea Yesu wakisema, “Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni?” Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, “Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi. Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je, Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?” Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”4_4″ _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

TAFAKARI

TUJIKABIDHI MIKONONI MWA MUNGU: Mungu anatutaka tuyafahamu mausia yake tupate kuwafahamisha wengine. Ezekiel anaambiwa ale, maana yake asome na kutafakari kwa kina mausia ya Mungu, na tukisha fahamu na kuwa na nguvu atutume kuwalisha wengine kwa mafunuo tunayoyafahamu. Utume wa malezi katika Kanisa umekuwa mgumu kwa sababu wengi hatutengi muda kusoma na kutafakari Neno la Mungu kwa kina. Tufahamu kuwa neno hilo, “Ni hai, lina nguvu, na linafahamu mpango wa Mungu kikamilifu” (Ebr 4:12-13). Tutenge muda kwa ajili ya Neno la Mungu.  Katika injili ya leo, Kristo anaweka mbele yetu utaratibu wa kufika katika utukufu wa Mungu Baba. Mwaliko ni kuwa wanyenyekevu, kujiachia mikononi mwa Mungu na kutegemea neema na huruma yake. Tuepe majivuno ya namna yeyote yanayotokana na nafasi tulizojaliwa kwa ajili ya huduma za Kanisa au za kijamii. Aidha, kama watoto wadogo, tuwe daima tayari kuongoka na kumrudia Mungu kwa unyofu wa moyo.

SALA: Ee Bwana utupe moyo ulio mnyofu kama watoto wadogo.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

You may also like these