[et_pb_section fb_built=”1″ theme_builder_area=”post_content” _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default”][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” column_structure=”2_5,3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”2_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 04/08/2024
2024 AGOSTI 4: DOMINIKA YA 18 YA MWAKA
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 2
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Somo 1. Kut 16:2-4, 12-15
Mkutano mzima wa wana wa Israeli uliwanug’unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuuwa kwa njaa kusanyiko hili lote. Ndipo Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni: na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo. Nimeyasikia manung’uniko ya wana wa Israeli; haya! Sema nao, ukinena, wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Ikawa wakati wa jioni; kware wakakaribia wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo. Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama sakitu juu ya nchi. Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Wimbo wa Katikati. Zab 78:3-4, 23-25, 54
1. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za Bwana na nguvu zake.
(K) Akawanyeshea mana ili wale; akawapa nafaka ya mbinguni.
2. Lakini aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni; Akawanyeshea mana ili wale Akawapa nafaka ya mbinguni. (K)
3. Mwanadamu akala chakula cha mashujaa; Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha. Akawapelekea hadi mpaka wake mtakatifu, Mlima alioununua kwa mkono wake mtakatifu. (K)
|
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Somo 2. Efe 4:17, 20-24
Nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao. Basi ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo, ikiwa mlisikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Injili. Yn 6:24-35
Mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernamu wakimtafuta Yesu. Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa? Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, ninyi mnanitafuta si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele. Ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na baba, yaani Mungu. Basi wakamwambia, tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, hii ndio kazi ya Mungu. Mmwanini yeye aliyetumwa na yeye. Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? Baba zetu waliila mana jangwani, kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. Yesu akawaambia Amin, amin, nawaambieni, siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, Bwana siku zote utupe chakula hiki. Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa naye aniaminie hataona kiu kamwe. |
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
TAFAKARI.
UIMARA WA KIROHO NI SULUHISHO KWA CHANGAMOTO ZA KILA SIKU Tuanze tafakari yetu kwa kujiuliza: Kwa nini tunamtafuta Mungu? Kwa nini tunasali? Je, imani yetu imejengwa katika nini? Uzoefu unatuonesha mara nyingi mwanadamu anapokuwa na hitaji ndipo humkimbilia Mungu. Mmoja ataomba kupata mtoto, mwingine kupata kazi, mwingine kupata uponyaji nk. Ukarimu wa Mungu hutujia na hapo tunafarijika. Lakini baada ya hali hii wengi humgeuzia kisogo Mungu au wakati mwingine hali ya kiimani hupungua. Muunganiko wetu na Mungu tunaupatia zaidi vionjo vya kidunia. Tunamkimbilia ili kutupatia chakula na mahitaji ya kimwili tu. Dominika ya leo inatualika katika safari ya kiroho, safari ambayo itatufanya tuunganike na Mungu katika ukamilifu wote kwani tunapoimarika kiroho hata changamoto za kila siku tutazikabili katika ukweli tukiwa na tumaini la kuwezeshwa na mwenyezi Mungu. Safari ya waisraeli kutoka utumwani Misri ambayo tunaelezewa katika somo la kwanza ilinuia kuwaandaa kiroho Waisraeli ili kuunganika kweli na Mungu. Katika safari hiyo tunaoneshwa taabu ya mwanadamu anayeshindwa kuitambua nia ya Mungu. Wao walibaki katika namna za kimwili na hivyo kwao ni bora kubaki katika utumwa ili mradi mkono unakwenda kinywani: “Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulivyokula vyakula hata kushiba…” Wanasahau mara moja kilio chao na ugumu wa utumwani kwa sababu tu wameona njaa; wanasahau mara moja jinsi walivyopoteza hadhi yao. Kumpitisha mwanadamu njia ngumu ili kuufikia uhuru wa kweli ni kazi ngumu. Namna hii ambayo hudai kujitoa, juhudi na sadaka huonekana kama kikwazo. Ndiyo maana wengi hata katika jamii yetu letu hukimbilia njia nyepesi kujipatia masuluhisho ya kimaisha. Wapo wengine wanaodiriki hata kuwatoa kafara watoto, ndugu au watu wa karibu ili kupata utajiri na madaraka. Watu hawa hawajitambui kuwa wamefanywa watumwa na mambo ya kidunia ambayo mara nyingi huwanyima furaha ya kweli na inayodumu. Wanahangaika kila leo kuhuisha mambo hayo ya giza kwa sababu si ya kudumu. Ni vigumu sana kwa watu waliofikia hali hii kuwarudisha na kuwapitisha jangwani mithili ya waisraeli; kwao ni bora kuendelea na utumwa wao wa kidunia. Katika Injili ya Dominika hii Kristo anaeleza umuhimu wa kubadili muelekeo huo. Anaanza kwa kuonya akisema: “Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika.” Onyo lake hili linatokana na namna watu aliowalisha walivyohangaika kumtafuta. Yeye alitambua kuwa wanamtafuta si kwa sababu wamepata njaa ya kiroho bali ni kwa sababu walikula na kushiba kimwili. Hawamtafuti kwa sababu wamekula na kushiba kiroho bali kwa sababu “walikula ile mikate wakashiba.” Ni shibe ya kimwili ndiyo inawasukuma kumtafuta Kristo. Wanavyomkumbushia jinsi baba zao walivyopewa chakula kutoka mbinguni kupitia Musa wanaonesha namna yao ya kumwona Kristo kama “Musa” mwingine aliyekuja kuwapatia chakula. Bado hawajapata msukumo wa kiroho. Mwaliko wa Kristo ni kufanyia safari ya kiroho ili kupata chakula cha kiroho, chakula ambacho kitawapatia nguvu ya kiroho. Pengine tunaweza kujiuliza sababu za msisitizo kutoka kinywani mwa Yesu kwa kushugulika na chakula cha kiroho. Chakula hicho ni nini? Na ipi ni tija yake kwa mwanadamu mzima? Kristo aliye kuhani wetu, yaani kiunganishi chetu na mwenyezi Mungu ndiye pekee anayetupatia chakula cha kiroho. Yeye ndiye chakula hicho kichukacho kutoka mbinguni. Msisitizo wake unatupeleka katika ukamilifu wa kazi ya Mungu ambayo inapaswa kumgeuza mwanadamu mzima, mwili na roho. Ukarimu wa Mungu unapaswa kutujenga kiroho. Hii inamaanisha kwamba, wema na ukarimu wake anaotukirimia kila siku ni nafasi kwetu na kutambua hakika ya uwepo wake na hivyo kuzikabili changamoto zote za kiroho na kimwili tukiwa na tumaini katika yeye. Tumaini hilo ndilo chachu ya uimara wa imani yetu na kichocheo cha maisha yetu ya kimaadili yanayopata maana katika ufunuo wake kwa njia ya mwanae Yesu Kristo Bwana wetu. Injili ya leo inaendelea kumdadavua Kristo kama hicho chakula cha kiroho ambacho tunapaswa kukihangaikia. Je, ni kwa nini chakula hicho kinapewa uzito? Sababu ya kwanza ni kwa sababu ya asili yake na muunganiko wake na Mungu. Chakula hicho kinapata nafasi ya kwanza kwa sababu kinaupatia ulimwengu uzima. Uzima huu unapaswa kutofautishwa na namna iliyozoeleka ya uzima. Ni uzima wa kimungu unaodumu milele: “Yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” Hivyo ni mwaliko wa kuuona wema wa Mungu na muunganiko wake na sisi, namna ambayo inaufanya uwepo wetu hapa duniani uwe ni wa matumaini. Chakula hicho cha kiroho kinatuelekeza katika matendo mawili muhimu. “Yeye ajaye kwangu” hii humaanisha yeye anayeacha namna yake, tamaduni zake na mazoea na kumfuata Kristo. Pili, “Yeye aniaminiye” ikimanisha paji la imani katika ufunuo wa Kristo. Hizi ni hatua mbili muhimu. Kristo anatutaka tutoke katika utu wetu wa zamani, yaani kusadaka na kufanya “metanoia” ya kweli. Maisha yetu katika imani ya kikristo ni mwanzo mpya. Namna na matamanio ya kidunia hayajatupatia suluhisho la kudumu. Kila mara tunajikuta tunahangaika kutafuta faraja nafsini mwetu. Tugeuke na twende kwa Yesu. Tendo hili la kumwendea Yeye ni tendo la kiimani na lenye mguso wa kiroho. Hivyo linahitaji paji la imani. Vinginevyo tutaingia katika hatari ya kumpokea Kristo kama mganga wa kienyeji ambaye tunamkimbilia tunapokuwa na shida tu na mambo yetu yanapokuwa sawia tunamsahau. Safari ya kiroho inadhihirika katika utu upya tunaouvaa kwa njia ya ubatizo. Mtume Paulo anatuasa sisi Wakristo kudhihirisha huo utu mpya. Mkristo hapaswi kuhangaika na kuridhika na mapaji mbalimbali au mema wapokeayo kutoka kwa Mungu mithili ya utamu wa manna waliyokula pale jangwani wana wa Israeli. Tukibaki katika namna hiyo ni sumu kwa maendeleo yetu kiroho na kizuio cha kuwa vyombo vya kuufunua upendo wa Mungu kwa wengine. Tunapouona mkono wa Mungu tunapaswa kusafiri katika namna ya kiroho na kuelewa maana yake; mkono wake unaotenda kazi kwetu unatupatia neema, utulivu na kutosheka. Unatuonesha upendo na kujali. Hayo ndiyo yanapaswa tuyatafute kwa bidii na kuyaeneza. Karamu ya kimwili itushibishe kwanza roho zetu na kutufanya tuwake ndani mwetu uwepo wa Mungu. Kubaki kufurahia mafanikio ya kimwili na yaonekanayo tu ni kushindwa kujivua utu wa kale. Namna hiyo inamfanya mmoja kuhangaika kumtafuta Mungu si kwa ajili ya kukua kiroho bali kwa ajili ya faida za kimwili. Changamoto nyingi za kimaisha zinaonekana kutopata mwarobaini wa kutosha kwa sababu ya mmoja kutuama katika masuluhisho yanayomjenga kimwili tu. Wema na ukarimu wa Mungu kupitia mapaji mbalimbali haumjengi mtu kufika hali kukua katika wema, upendo, huruma, ushirikiano, ukarimu na fadhila nyingine nyingi. Tunu za kimungu tuzipatazo kwa njia ya imani ni nyenzo ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha.
SALA: Ee Yesu utulishe na kutunywesha kwa Mwili na Damu yako Takakatifu.
|
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]