Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 17/07/2024

2024 JULAI 17: JUMATANO-JUMA  LA 15 LA MWAKA

Mt. Pambo, Mkaa Pweke
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma 3

Somo 1. Isa 10:5-7, 13-16

Bwana asema hivi: Ole wake Ashuru! Fimbo ya hasira yangu, ambaye gongo lililo mkononi mwake ni ghadhabu yangu! Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani. Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache. Kwa maana amesema, kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa. Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kioto cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia. Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti. Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, atawapelekea kukonda watu wake walionona; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto.

Zab 94:5-10, 14-15

1. Ee Bwana wanawaseta watu wako;
Wanauseta urithi wako;
Wanamwua mjane na mgeni;
Wanawafisha yatima.

(K) Bwana hatawatupa watu wake.

2. Nao husema Bwana haoni;
Mungu wa Yakobo hafikiri.
Enyi wajinga miongoni mwa watu fikirini;
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili? (K)

3. Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asione?
Awaadhibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue? (K)

4. Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake.
Wala hatauacha urithi wake,
Maana hukumu itairejea haki,
Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata. (K)

Injili. Mt 11:25-27

Wakati ule Yesu alijibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

TAFAKARI.

HEKIMA YA MUNGU: Nabii Isaya anaiashiria Asiria kama shoka mkononi mwa mtumiaji, mtumiaji wa Asiria ni Mungu. Ndiye aliyeiinua kama mwenye shamba anavyoliinua chipukizi katika shamba lake. Mungu anaitumia Asiria kuisafisha Yuda, mfano wa Wasiria unatumika kwa Wayuda ili wafanye toba. Wakati huu Asiria ikawa na majivuno ikidhani imekuwa na uweza na mafanikio. Hili lilimpelekea nabii Isaya kuikumbusha Asiria nafasi yake, akiwaambia, bila uweza wa mikono ya mtumia shoka, shoka halina kazi. Ilikuwa bure kwa Asiria kujivunia uweza na ushindi wake, bila kumpa Mungu nafasi. Ilipaswa ijinyenyekeshe mbele ya Mungu. Unyenyekevu unahimizwa na Kristo katika sehemu ya Injili ya leo. Waliofichwa wenye hekima na akili ya kiulimwenguni tofauti na watoto wachanga wanaobakia wanyoofu, wanyenyekevu na tayari kutii maelekezo. Waisraeli walialikwa kuitambua Hekima ya Mungu muda wote. Hekima ya Mungu ndiyo iliyotumika kumtuma Nabii Isaya awaonye na kuwaalika kufanya toba. 

Sala: Ee Bwana neema yako ituwezesha kuendelea kutambua hekima yako, kuipokea na kuiishi.

Masomo ya Misa Oktoba 12

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 12/10/2024 2024 OKTOBA 12: JUMAMOSI-JUMA LA 27 LA MWAKA Mt. Wilfridi wa York, AskofuRangi: KijaniZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 3:22-29 Andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile...

Masomo ya Misa Oktoba 11

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 11/10/2024 2024 OKTOBA 11: IJUMAA-JUMA LA 27 LA MWAKA Mt. Yohane wa XXIII, PapaRangi: KijaniZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 3:7-14 Fahamuni basi, yakuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. Na andiko, kwa vile...

Masomo ya Misa Oktoba 10

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 10/10/2024 2024 OKTOBA 10: ALHAMISI-JUMA LA 27 LA MWAKA Mt. Daniel Komboni, Askofu MmisionariRangi: NyeupeZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 3:1-5 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo...

Masomo ya Misa Oktoba 9

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 09/10/2024 2024 OKTOBA 9: JUMATANO-JUMA LA 27 LA MWAKA Mt. Dionisi, Askofu na Wenzake, Mashahidi/ Mt. Yohane Leonardi, PadreRangi:KijaniZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 2:1-2, 7-14 Baada ya miaka kumi na minne, nalipanda...

Masomo ya Misa Oktoba 8

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 08/10/2024 2024 OKTOBA 8: JUMANNE-JUMA LA 27 LA MWAKA Mt. ReparataRangi:KijaniZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 1:13-24 Mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu...

Masomo ya Misa Oktoba 7

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 07/10/2024 2024 OKTOBA 7: JUMATATU-JUMA LA 27 LA MWAKA Bikira Maria Mt. Mama wa RozariRangi: NyeupeZaburi: Juma IIISOMO 1. Gal 1:6-12 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na...

Masomo ya Misa Dominika ya 27

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 06/10/2024 2024 OKTOBA 6: DOMINIKA YA 27 YA MWAKA Rangi: KijaniZaburi: Juma IIISOMO 1. Mwa 2:18 – 24 Bwana Mungu alisema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanya msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akafanyiza...

Masomo ya Misa Oktoba 5

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 05/10/2024 2024 OKTOBA 5: JUMAMOSI-JUMA LA 26 LA MWAKA Mt. Faustina Kowalska, BikiraRangi: KijaniZaburi: Juma IISOMO 1. Ayu 42: 1-3, 5-6, 12-17 Ayubu alimjibu Bwana na kusema, najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,...

Masomo ya Misa Oktoba 4

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 04/10/2024 2024 OKTOBA 4: IJUMAA-JUMA LA 26 LA MWAKA Fransisko wa AsiziRangi: NyeupeZaburi: Juma IISOMO 1. Ayu 38:1, 12-21, 40:3-5 Ndipo Bwana alimjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Je! Umeiamuru asubuhi...

Masomo ya Misa Oktoba 3

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 03/10/2024 2024 OKTOBA 3: ALHAMISI-JUMA LA 26 LA MWAKA Wat. Ndugu Ewaldi, WafiadiniRangi: KijaniZaburi: Juma IISOMO 1. Ayu 19:21-27 Ayubu alisema: “Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu...