Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 16/07/2024
2024 JULAI 16: JUMANNE-JUMA LA 15 LA MWAKA
Bikira Maria Mt. wa Mlima Karmeli
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 3
[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”3_5″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/07/saint-writeups-7-1080×675-1.png” _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”saint-writeups-7-1080×675″ hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” type=”4_4″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.26.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]
Somo 1. Isa 7:1-9
Ilikuwa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda. Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswayo na upepo. Basi Bwana akamwambia Isaya, “Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja wa dobi. Ukawaambie,” Angalia, ukatulie; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia. Kwa kuwa Shamu amekusudia mabaya juu yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia, wakisema, haya, na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli. Bwana Mungu asema hivi,” Neno hili halitasimama wala halitakuwa.” Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena; tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka hamtathibitika. |
Wimbo wa Katikati. Zab 48:1-7
1. Bwana ndiye aliye mkuu,
(K) Mji wa Mungu wetu ataufanya imara hata milele. 2. Mlima Sayuni pande za kaskazini, 3. Maana, tazama, wafalme walikusanyika; 4. Papo hapo tetemeko liliwashika, |
Injili. Mt 11:20-24
Yesu alianza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.”Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Taro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.” |
Tafakari.
IMANI YAKO IKIWA IMARA UTAKUWA IMARA: Tenne Williams aliandika mchezo mmoja aliouita Usiku wa Iguana. Katika eneo moja la huo mchezo Anna Jelke anaongea na Shannon, anayeonekana kuwa na tatizo la kutumia vilevi na kulewa. Anna anasema “Vilevi sio tatizo lako ewe Shannon.” Ndugu Shannon anamwambia Anna, Hivyo ni nini tatizo langu? Anna akasema, “Jambo la zamani sana huku duniani – ni umuhimu wa kuamini katika jambo fulani au mtu fulani – karibu kila mtu – karibu kila kitu … kitu fulani.” Imani katika maisha yetu ni sawa na msingi imara kwa nyumba. Imani ni kitu imara ambacho kinakuwa msingi imara wa kitu kingine. Kama imani yetu ikiwa imara, maisha yatakuwa imara. Kama imani yetu ikiwa ya mashaka na maisha yetu yanakuwa ya mashaka mashaka. Tukihitaji maisha imara tuwe na imani imara. Tujitahidi kustawi katika imani na kuwa tayari kufanya toba ya kweli. Sala: Ee Bwana neema yako ituwezeshe kustawi katika imani.
|