Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 15/07/2024
2024 JULAI 15: JUMATATU-JUMA LA 15 LA MWAKA
Mt. Bonaventura, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 3
Somo 1. Isa 1:10-17
Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora. “Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani?” Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; che siifurahi damu ya ng’ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume. Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu? Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua. Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; chene kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. |
Wimbo wa Katikati. Zab 50:8-9, 16-17, 21, 23
1. Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, (K) Nitamwonyesha wokovu wa Mungu. 2. Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, 3. Ndivyo ulivyofanya, nami nitanyamaza, |
Injili. Mt 10:34-11:1
Yesu aliwafundisha mitume wake: “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga, kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.” Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake. Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. |
TAFAKARI
TUSIKILIKIZE DHAMIRI ZETU NJEMA: Kati ya urafiki mkubwa sana uliotajwa katika Maandiko Matakatifu ni urafiki kati ya Jonathani na Daudi. Urafiki huo unakuwa wa pekee na waajabu kwa sababu mfalme Sauli ambaye ni baba yake Jonathani alimchukia Daudi. Sauli alitaka kumuua Daudi, akamwambia Jonathani amsaliti. Jonathani alikataa. Inapofikia wakati wa kufanya lililo sahihi au lililo baya sio wazazi au marafiki wa karibu sana watakaotufanya tuenende kinyume na dhamiri zetu. Hilo ndilo la muhimu Kristo analolisisitiza katika Maandiko Matakatifu ya leo. Kwa kujitoa kwake Kristo, Mwana wa Mungu anawagawa watu, hata baba na mwanae au mama ad obi yake kwa misingi hii ya kila mmoja kujiweka tayari kusimamia dhamiri yake akijishikamanisha na lililo jema na sahihi. Uamuzi wa kumfuata Kristo unagusa mtima wa maisha ya mtu, hakuna mtu anayepaswa kuingilia sehemu hiyo au maamuzi hayo, sio baba wala mama wala rafiki wa karibu. Sala: Ee Bwana uniwezeshe kusimamia lililo jema muda wote bila kujali wengine wanafikiria nini. |