Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 28/05/2024
2024 MEI 28 : JUMANNE-JUMA LA 8 LA MWAKA
Mwenyeheri Margaret Pole
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 3
Somo 1. 1 Pet 1:10-16
Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” column_structure=”1_2,1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/bible-study_SQ-scaled-1.jpg” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” title_text=”bible-study_SQ-scaled” animation_style=”bounce” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][et_pb_column _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” type=”1_2″ theme_builder_area=”post_content”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” theme_builder_area=”post_content” hover_enabled=”0″ sticky_enabled=”0″]Wimbo wa Katikati. Zab 98: 1-4
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, (K) Bwana ameufunua wokovu wake. 2. Bwana ameufunua wokovu wake, 3. Miisho yote ya dunia imeuona |
Injili. Mk 10:28-31
Petro alimwambia Yesu, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza. |
TAFAKARI
FAIDA ZA UFUASI WA KWELI: Injili ya leo ni mwendelezo wa Injili ya jana. Baada ya jana Yesu kutoa katekesi kuhusu kujitenganisha na malimwengu kwa ajili ya uzima ujao, leo mtume Petro anahoji faida za kujitenganisha na vitu vya ulimwengu huu ni zipi. Kwa maelekezo yake yeye ni mmojawapo wa walioacha vyote wakamfuata Yesu. Anauliza atafaidikaje kwa kumfuata na kuacha vyote? Jibu la Yesu kwa Petro linamfundisha yeye na sisi kuwa vyote tunavyoacha sasa kwa ajili ya Mungu ni hazina yetu ya sasa na ya baadaye. Kwa maneno mengine vile tunavyoacha sasa kwa ajili ya Mungu havipotei bali “tunamkopesha Mungu” na atatulipa vyote sasa na baadaye. Pamoja na utamu utokanao na riba anayotoa Mungu kwetu, Yesu anatukumbusha kuwa zipo gharama za ufuasi na gharama hizo ndiyo udhia anaomwambia Petro. Leo Yesu anataka nimfuate kama alivyowaita mitume wakamfuata nasi tunaitwa vivyo hivyo na anatuhakikishia upendo tunaomwonesha hautapotea kamwe. |
Sala: Ee Yesu unijalie ujasiri wa kukufuata bila ya kujibakiza. |