Masomo ya Misa Mei 20

[et_pb_section fb_built=”1″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_row column_structure=”3_5,2_5″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”3_5″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/Moc-Blog-Header410201991513AM.png” title_text=”Moc-Blog-Header410201991513AM” _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” hover_enabled=”0″ global_colors_info=”{}” sticky_enabled=”0″][/et_pb_image][/et_pb_column][et_pb_column type=”2_5″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” hover_enabled=”0″ global_colors_info=”{}” sticky_enabled=”0″]

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 20/05/2024

2024 MEI 20 : JUMATATU-JUMA LA 7 LA MWAKA

Bikira Maria Mama wa Kanisa
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 7

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”4_4″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Somo 1. Yak 3: 13-18 (Masomo ya Sherehe Mwa 3:9-15, 20)

N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row column_structure=”1_2,1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Wimbo wa Katikati. Zab 19: 7-10 au Zab 87:1-2, 3 na 5, 6-7)

1. Sheria ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa Bwana ni amini,
Humtia mjinga hekima.

(K) Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.

2. Maagizo ya Bwana ni ya adili,
Huufurahisha moyo.
Amri ya Bwana ni safi,
Huyatia macho nuru. (K)

3. Kicho cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu milele.
Hukumu za Bwana ni kweli,
Zina haki kabisa. (K)

4. Ni za kutamanika kuliko dhahabu,
Kuliko wingi wa dhahabu safi.
Nazo ni tamu kuliko asali,
Kuliko sega la asali. (K)

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”4_4″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

Injili. Mk 9:14-29 au Mk 10:17-27)

Yesu na Petro na Yakobo na Yohane walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Akawajibu, akasema, Enyi  kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaaanguka chini; akagaagaa, akitokwa na povu. Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua; naye akasimama. Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][et_pb_row column_structure=”1_2,1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_text _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”]

TAFAKARI

IMANI NA SALA VINAPONYA: Tumesikia katika Injili jinsi Mitume walivyoshindwa kumtoa pepo. Upungufu wa imani na kutosali vilisababisha washindwe kumtoa pepo. Hali hii ya kushindwa ilisababisha mahangaiko na mkato wa tamaa kwao na kwa baba wa kijana huyu. Baba wa kijana anamwomba Yesu amponye mwanae. Alitambua kuwa alikuwa na udhaifu ambao ni mashaka ila alikabidhi mashaka hayo kwa Yesu akaamini katika nguvu ya uponyaji ya Yesu. Kwa kuona imani yake Yesu anamponya kwanza yeye kwa kumwondolea mashaka yake kisha anamponya kijana wake kwa kumtoa pepo. Tujifunze kuwa kabla ya kutenda jambo lolote tunapaswa kuamini na kusali tukiomba msaada wa Mungu kwa lile tunalotaka kutenda.  Tuwe na mazoea mazuri ya mazoezi ya kiroho hasa kufunga na kusali tuweze kuchota nguvu za kutenda mambo makubwa ya kiimani. Leo hii wapo wanaoshindwa na maovu mbalimbali kama vile uongo, ulevi, uzinzi, uasherati, wivu, na uvivu kwa sababu tu hawajaweka nguvu katika sala ili kushinda vilema hivyo. Tukiamini na tukisali tutashinda yote.

SALA: Ee Bwana Yesu tunaomba utuongezee imani.

[/et_pb_text][/et_pb_column][et_pb_column type=”1_2″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” global_colors_info=”{}”][et_pb_image src=”https://claretianpublications.or.tz/wp-content/uploads/2024/05/tumblr_lzp3x6n7do1qggdq1.jpg” title_text=”tumblr_lzp3x6n7do1qggdq1″ _builder_version=”4.25.0″ _module_preset=”default” animation_style=”bounce” global_colors_info=”{}”][/et_pb_image][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these